MSOMAJI HII NI STORY YA KUSISIMUA YA BWANA ERICK MOSHA AMBAE AMEPATA
SHIDA SANA KATIKA MAISHA YAKE AKIWA KATIKA SAFARI YA KUTAFUTA ELIMU MKOANO DODOMA.INALIZA SANA
Ilikua ni asubuhi na mapema
ubaridi unaopuliza katika mkoa wa na upepo wa msimu katika mkoa wa Kilimanjaro.
Ambapo mama erik na mwanae wakiwa wapo katika hali ya majonzi katika kuagana
kwani kijana Erick alikua anaelekea mkoani Dodoma kwa masomo baada ya kupata nafasi ya
kusomea uwalimu kwatika chuo hicho
Mama erik nenda mwanangu
kasome maana elimu ndio kila kitu katika maisha yako (huku akilia )maisha ni
magumu sana mwanangu unatakiwa ujitume kadri uwezavyo nitajitahd kuuza ndizi
ili usome mwanangu..
Erick nimekuelewa mama yangu nitajituma mama sema najickia vibaya
mama kukuacha katika hii hali ya upweke nani atakusaidia hata kukatia majani au
kulisha ng`ombe zetu mama yangu?
Mama Erick mwanangu usiniofie mimi huku (akfuta machozi)
Erick sawa mama yangu ila nitakukumbuka sana lakin hatuna budi mama
baki salama
Mama alinipa elfu ishirini kama
nauli ya mimi kutoka pale kuelekea chuoni udom kwani huko nilipanga kufikia kwa
mjomba wangu alieitwa Joshua moshi
kwani ndie angekua mwenyeji wangu kabla ya kufika chuo. Nakumbuka niliondoka
siku ile ndo ilikua mara ya mwisho kumuona mama yangu kipenzi ambae mpaka leo
namkumbuka kwani ndie muhimili wangu wa pekee…
Nilibaatika kuzaliwa peke yangu
na kulelew na mzazi mmoja Baba yangu aliuwawa wakati bado nikiwa mdogo sana
nikiwa na umri wa miaka miwili.siijui raha ya kuwa na baba kama watu wengine. Nililelewa
na mama kwa kipindi chote hali ya kuwa hali ya nyumbani ilikua ngumu kwani mama
yangu hakuopataga bahati ya kusoma katika uschana wake hivyo alikua mama wa
nyumbani na alijitoa sana katika malezi yangu hasa kwenye swala la elimu mama
yangu alikuwa akinisih nisome sana ili nikomboe maisha ya nyumbani na kufkia
ndoto zangu kwa ujimla.
Nilitoka moja kwa moja nikimuaga
mama na kwenda moja kwa moja ambapo nilidandia tatu (daladala)ilionifikisha
mpaka njia panda ya machame ambapo
nlisubiri gari znazotoka boma znazoelekea mkoani Dodoma ili kufika kwa mjomba joshua
tyr kwa maandalizi ya masomo yangu
Nakumbuka nikiwa njiani nilijinyima
kula hali ya kuwa gari nliopanda ilikua mbovu na inasimama mara kwa mara
kutokana na ubovu wa safari hiyo.Nilifika mkoani Dodoma majira ya saa 2 usiku
nikiwa na njaa sana moja kwa moja
nlielekea katika taxi kadhaa ambazo zilikua karibu na stendi ya mkoa wa Dodoma ambapo
niliulizia dereva aitwae Joshua mosha
kwakua nilikua sina hata simu ya mawasiliano
Kwakua mjomba wangu alikua dereva
na alikua maarufu kidogo maeneo hayo
haikua tabu kumpata.Baada ya nusu saa hivi mjomba alifika na alionekana akiwa
amelewa akijipiga kifua “jombaa langu limekuja mweshmiwa wa baadae toto pekee
la dada yangu” alioneshwa kufurai sana kutokana nay eye na mama yangu kupendana
sana . “shkamoo mjomba “ nilimsalimia
lakin alinijibu “shkamoo makelele “ Erick twende zetu kwanza ukapumzike
umechoka na safari mimi nina ofa za bia nimeacha huko “ sikumjibu chochote bali nilionyesha sura ya kukubaliana
na wazo lake ambapo nilipanda TAXI yake kuu kuu Nakumbuka sana siku ile katika
maisha yangu ni siku ambayo sitaisahau katika maisha yangu ilikua ni may 16 mwaka 2014 laiti ningejua
kama ile siku ingekua vile basi nisinge
hangaika kuitafuta elimu ningalibaki mgombani tu na mama yangu kipenzi.
Tukiwa na mjomba Joshua tunatoka
maeneo ya standi ya mkoa Dodoma nikiwa mgeni kidogo nakumbuka tulielekea magharibi kidogo na stendi mbele kidogo na
shule ya sekondari Dodoma na mbele
kidogo ya Bunge la nchi yetu kulikua na mtaa unaitwa makole kama skosei ndipo
tulismamishawa na watu wawili ambapo walikua na mwonekano kama abiriA kwakua nilikua nimekaa siti ya mbele pembeni
na dereva mjomba aliamua kusmamisha gari
“tusiache vichwa pesa ya kufunga
hesabu hii mwanangu” aliyasema mjomba
huku akisimamisha gari wale watu walifinguA mlango na kuingia ndani ya gari walidai kuwa
wanataka kuelekea eneo la area d maeneo ya karibu na mlima walitaka kujua bei
mjomba aliwambia waandae elfu 5000 maana hata sisi tulikua tukielekea maeneo hayo
hayo bila kusita gari ilirudi tena
barabarani na kuanza kuelekea palipotakiwa
Lakini tukiwa njiani Yule abiria
wa kiume alipiga simu na kuongea maneno ambayo yalintisha kidogo
“mkuu mzigo tunio lakini viumbe
ni viwili andaa mazingira “ kasha akakata simu bila kupata majibu kwa
aliempigia au mwitikio lakini sikujali
na nikaendelea kuutazama uzuri wa mkoa wa Dodoma nakumbuka mjomba aliuliza hali ya mama na watu
wengne ambao walikua marafiki pale kijijin alionesha uchangamfu mkubwa pia
Nadhani ni kutokana na pombe ilio kichwani.
Tukiwa eneo la ukimya na kama
pori eneo ambalo liliitwa area d ghafla tuliona watu watatu wamesimama na kujitandaza
barabarani ghafla abiria tuliokua nao kwenye
gari wote wawili wakituambia kwa sauti “simamisha gari mpo chini ya ulinzi”
mwanamkwe alimnyooshea njomba silaa ndogo ya moto na Yule mwanaume alitoa panga
ambalo aliliweka usawa wa shingo yangu
nilishtuka sana
“hapa asimamishi gari mtu na leo mmekosea namba nasema labda tufe woote” aliyasema hayo maneno mjomba huku akiongeza
spidi ya gari straight kuelekea pale wale watu watatu walikua wamesimama kulizinga gari . nikiwa nimeshikwa na butwaa
na nikiusoma mchezo unavokua nakumbuka
wale watu baada ya kuona gari inakuja speed na hakuna dalili ya kusmama
waliamua kutoka barabani
“neema uwa huyo mshenzi fyatua ya
utosi tumalizee” ilikuz ni sauti ya Yule mwanaume ghafla gari lilipoteza uelekieo na
kuingia porini katika zile purukushani za vitisho. Nikiwa nmapigo ya moyo
yanaenda mbio na nikijishkilia vizuri kutokana na kuyumba na mwendo kasi wa
gari niliskia kishindo kikubwa sana
katika maskio ambacho kilipelekea
mvurugano ndani ya gari …..sikumbuki
nini kilitokea lakini nlikua nipo chini navuja damu maeneo ya shingo na maumiv
makali pia. Nilinitahd kuinuka lakn nilishindwa nilijarib kugeuza kichwa pia
niliskia maumivu makali sana . nilijaribu kupaza sauti kuomba msaada lakin
niliskia maumiv makali shingoni na pia sauti haikutoka.. nilibaki natokwa na
machozi huku nikiwa najihisi kama maskio yangu yameziba………
Mpendwa msomaji usikose sehemu ya pili ya mkasa huu wa kweli wa Erick mosha